Ripoti kutoka Ufukwe wa Magharibi unaokaliwa na Israel zinasema kuwa ukaguzi wa awali wa mwili wa kijana wa Kipalestina aliyeuwawa juma hili mitaa ya mashariki ya Jeusalem, unaonesha kuwa kijana huyo alichomwa moto akiwa hai.
Wakuu wa Israel wanasema hawajui hasa vipi kijana huyo wa miaka 16 aliuwawa.
Familia yake inaamini aliuliwa kulipiza kisasi mauaji ya vijana watatu wa Israel mwezi uliopita.
Shirika la habari rasmi la Palestina (Wafa) lilimnukuu mkuu wa sheria akisema kuwa 90% ya mwili wa Mohammad Abu Khdair ulikuwa umeteketea.
Shirika hilo linaripoti kuwa afisa wa Palestina alikuwako kwenye ukaguzi huo wa matabibu, na jivu lilikutikana ndani ya kifua cha Abu Khdair ambayo inamaanisha alivuta moshi wakati akiuungua, yungali hai.
Saturday, July 5, 2014
Ukaguzi wa awali waonesha kijana aliyeuwawa Ufukwe wa Magharibi alichomwa moto akiwa hai
Labels:
News