Vikosi vya serikali Somalia vimefanikiwa kuidhibiti upya ikulu ya rais katika mji mkuu Mogadishu baada ya wapiganaji wa Al Shabaab kuishambulia.
Maafisa wanasema washambuliaji wapatao watano kutoka kundi la al-Shabab - waliuawa walipoingia katika eneo la ikulu hiyo.
Washambuliaji hao wanadaiwa kulipua bomu lililotegwa kwenye gari karibu na langu kuu la Ikulu hiyo.
Waziri wa habari na mawasiliano wa Somalia Mustaf Dhuhulow ameambia BBC kuwa tayari mmoja wa washambuliaji hao amekamatwa na anahojiwa na polisi.
Waziri Mustaf amesema, '' Walishambulia ikulu ya rais saa za jioni. Alikuwa watu washambuliaji watatu pamoja na dereva wao.
Washambuliaji hao waliuawa lakini dereva wao alipata majeraha madogo na anazuiliwa na polisi na kuhojiwa.
Walijaribu kuvamia Villa Somalia lakini wakakomeshwa. Tutawapa maelezo zaidi baadaye. Na tutaweza kutoa maelezo zaidi kwa raia wa Somalia na dunia nzima.''
Hii ni mara ya pili kwa Al Shabaab kuvamia ikulu ya rais mjini Mogadishu mwaka huu japo mara ya kwanza walifanikiwa kuingia ndani.
Rais Hassan Sheikh Mohamoud hakuwepo wakati wa shambulio hilo.
Kundi la wapiganaji wa kiislamu Al shabaab limefukuzwa kutoka mjini Mogadishu tangu mwaka wa 2011 lakini limekuwa likifanya mashambulio ya kuvizia tangu wakati huo.
Wanamgambo hao wanaaminiwa kufanya mashambulio kadhaa pia katika nchi jirani ya Somalia kama vile Kenya, Uganda na Tanzania kama njia ya kulipiza kisasi kwa kuingia majeshi ya Umoja wa Afrika nchini Somalia.
Popular Posts
-
New Music: Professor Jay ft J Hustle and Nigga J - 3 Chafu
-
Download wimbo Kamili HAPA MKITO wa Msanii mdogo wa Umri Mkubwa wa akili aka "Jose G" akiwa amemshirikisha Legendary SpacDaw...
-
New Music: Chidi Benz Feat Bob Junior - Mahaba Niuwe
-
The third installment of the popular The Expendables movie franchise won't hit theaters until August 15th, but a near perfect copy has ...
-
1. Transformers: Age of Extinction A mechanic and his family join the Autobots as they are targeted by a bounty hunter from another wor...
-
Meet Corazon Kwamboka from Kenya,which i prefer to call MISS B00TY,she’s beautiful and voluptuous, check out her stunning photos After ...
-
New Music: Monii ft Roma & GodZilla - Hatuhesabu Masaa
-
Men have to love the fact that twerking has gone from the hood other countries around the world. I just hope they don't think Miley Cy...
-
Baadhi wanawake siku hizi wamekuwa wakijiuliza vazi gan ambalo linafaa kuvaliwa wakati wa usiku na likawapendeza sasa unaweza kutazama pic...
-
Beef ya mastar wa Nigeria inaonekana bado haijaisha baada ya Davido kuzungumzia kitu gani kilimkasirisha hadi bifu na Wiz Kid kutokea, Wiz...
Advertisement
Advertisement
Advertisement With Us