Select Menu

Ads

Random Posts

Powered by Blogger.

Design

Technology

Circle Gallery

Shooting

Racing

News

Bottom

Thursday, July 17, 2014

Baada ya collabo na Chris Brown, WizKid athibitisha kufanya wimbo na Rihanna

Wizkid anazidi kuwapa sabababu za kutabasamu mashabiki wake ambao wamekuwa wakiziona picha zake instagram akiwa na mastaa kama Justin Bieber, Chris Brown, Rihanna na Karrueche Tran. 
Mwezi mmoja baada ya kueleza kuwa Rihanna amemuita ‘amazing’, mwimbaji huyo amethibitisha kuwa waliingia studio na kufanya wimbo. 

Wizkid amefunguka wakati akifanya mahojiano na Beat FM kupitia Toolz ambapo walitaka kufahamu kuhusu alichokifanya Marekani.  
Kabla ya Rihanna tayari Wizkid ameshafanya wimbo na Chris Brown. Uhusiano wake na Chris ndio uliompa connection na Rihanna, so inaonekana Rihanna na Chris wanapiga story kishikaji kwa mtazamo huo.