Wakati muigizaji Zendaya Coleman akishindwa kuvumilia mashambulizi ya mashabiki wa Aaliyah na ukosoaji wa familia ya muimbaji huyo na kuachana na mpango wa kuigiza filamu ya maisha yake, muigizaji Alexandra Shipp amchukua nafasi hiyo.
Alexandra ni muigizaji aliyeingia kwenye tasnia ya filamu tangu akiwa mdogo kama ilivyokuwa wa Zendaya na amewahi kushiriki episodes za ‘Switchd at Birth’, ‘Awkward’ na ‘Ray Donovan’.
Tangazo la kushirikiwa kwa Alexandwa lilitangazwa pamoja na waandaaji watendaji wa filamu hiyo, kampuni ya Wendy Williams.
Hata hivyo, familia ya Aaliyah ilijitokeza na kulaani filamu iliyopewa jina la Aaliyah: Princess of R&B kwa madai kuwa Lifetime haikuwa na vigezo vya kutosha kutengeneza simulizi la Aaliya. Inaripotiwa kuwa tayari familia hiyo imekodi mwanasheria kupinga hatua hiyo.
Saturday, July 19, 2014
Baada ya Zendaya kujitoa, Alexandra Shipp achukua nafasi ya kuigiza maisha ya Aaliyah
Labels:
Entertainment,
Movie