Muigizaji wa kike maarufu, Shannon Guess Richardson, jana (July 18) amehukumiwa kifungwa cha miaka 18 jela baada ya kukutwa na hatia ya kumtumia rais wa Marekani Barack Obama barua yenye sumu.
Muigizaji huyo alikamatwa June, 2013 baada ya kutuma barua hiyo yenye sumu ambayo ilielekezwa pia kwa Mayor wa New York Michael Bloomberg na mwanasheria anahusikana na udhibiti wa silaha.
Kwa mujibu wa ripoti ya uchunguzi, barua hiyo ilikuwa imebeba sumu kali aina ya ricin inayotengezwa kutokana na mbegu za mimea.
Uchunguzi unaonesha kuwa aliagiza mbegu hizo kwa njia ya mtandao na akajifunza jinsi ya kuzigeuza kuwa sumu kisha kutekeleza nia yake.
Muigizaji huyo ambaye alijifungua akiwa mahabusu alijitetea mahakamani hapo na kudai kuwa yeye sio mtu mbaya na hakuwa na nia ya kumuumiza mtu yoyote na kwamba vilivyoko kwenye barua hiyo sio vya kwake.
“I never intended for anybody to be hurt. I'm not a bad person. I don't have it in me to hurt anyone.”
Shannon mwenye umri wa miaka 36 ni mkazi wa Texas Marekani na ameigiza series maarufu za TV kama The Vimpire Diaries, The Blind Side na filamu ya The Walking Dead.
Pamoja na kifungo cha miaka 18 jela, muigizaji huyo ameamrishwa kulipa fidia ya $367,000.
Chanzo: The Independent
Saturday, July 19, 2014
Muigizaji wa The Vampire Diaries aliyemtumia rais Obama Barua yenye sumu afungwa jela miaka 18
Labels:
Entertainment,
News