Select Menu

Ads

Random Posts

Powered by Blogger.

Design

Technology

Circle Gallery

Shooting

Racing

News

Bottom

Saturday, July 19, 2014

Kuhusiana na Ndege iliyobeba wanajeshi wa Marekani yatua kwa dharura barabarani Uganda

Wakati ulimwengu ukiwa katika majonzi baada ya kuripotiwa kudunguliwa kwa ndege ya Malaysia, habari kutoka Uganda zinaeleza kuwa ndege iliyokuwa imebeba wanajeshi wa Marekani ililazimika kutua kwa dharura barabarani. 

Msemaji wa jeshi la polisi la Uganda, Phillip Mukasa amesema ndege hiyo ndogo ilikuwa imebeba watu nane ikiwa ni pamoja na wafanyakazi wawili na ililazimika kutua kwa dharura katika mji wa Mityana, kilometa 67 kutoka Kampala.

Ameeleza kuwa ndege hiyo ilikuwa imekaribia Sudan Kusini lakini kutokana na kupungukiwa mafuta rubani aliamua kurudi Uganda katika uwanja wa ndege wa Entebbe. 
Hakuna mtu aliyeumia katika tukio hilo na ndege hiyo haikupata uharibifu mkubwa