Beyonce Knowles amechochea kuni katika moto wa tetesi za usaliti wa mapenzi wa Jay Z baada ya kubadili kidogo mashairi ya wimbo wake ‘Resentment’ uliopo katika albam yake ya B’Day aliyoitoa mwaka 2006.
Wakati anaimba Resentment kwenye On The Run Tour, huko Ohio alibadili miaka inayoitaja kwenye wimbo halisi na kuitaja miaka ya uhusiano wake na Jay Z, yaani alitoa miaka 6 na kuwa 12 katika wimbo huo wenye kilio cha usaliti.
Kitendo hicho kilizua shangwe zaidi kutoka kwa mashabiki waliofahamu kabisa kuwa mwaka 2002 enzi za Bonnie&Clyde ndio mahusiano ya wawili hao yalichipua.
Wimbo halisi unasema: "Been ridin' with you for six years why did I deserve/ To be treated this way by you.” Lakini Beyonce alibadili miaka na akasikika akiimba:
"I know she was attractive but I was here first/ Been ridin' with you for 12 years why did I deserve/ To be treated this way by you, you/ I know your probably thinking what's up with Bee/ I been crying for too long what did you do to me."
Hata hivyo, wanandoa hao huonekana wakiwa wenye furaha na mtoto wao kila baada ya show zao.
Wednesday, July 2, 2014
Mbali na ugomvi kuwapunguzi fans, Beyonce achochea moto tetesi za usaliti wa Jay Z, abadili mashairi ya wimbo na kumlilia
Labels:
Entertainment,
Love Zone