Select Menu

Ads

Random Posts

Powered by Blogger.

Design

Technology

Circle Gallery

Shooting

Racing

News

Bottom

Wednesday, July 2, 2014

Linah aeleza kinachoendelea kumuweka mjini bila kuwa na nyimbo mpya na shows

Ndege Mnana, Linah ambaye kwa muda mrefu amekuwa kimya bila kuachia wimbo mpya kabla ya kuachia remix ya wimbo wa Kizaizai wa Diamond ameeleza sababu zinazomfanya aendelee kuishi maisha mazuri hata anapokuwa hana wimbo mpya redioni kiasi cha kupunguza mfululizo wa shows.

Linah amefunguka katika Power Jams ya East Africa Radio leo kuwa sababu kubwa inayomfanya aendelee kung’aa mjini hata bila shows wala kuwa na nyimbo mpya ni kujipanga mapema kuikabili hali yoyote itakayojitokeza kwenye maisha yake kama mwanamuziki. 

Labda niseme kitu kimoja, unajua unapokuwa msanii unatakiwa ujipange vya kutosha. Anything can happen. Kwa hiyo unapofanya kazi at the time unapokuwa vizuri inabidi ujipange kwa maisha ya mbele pia. Kama mimi nilikuwa nimejipanga enough kwamba in case ikitokea kitu chochote mimi niko sawa. Yaani sitatetereka.

Amesema anajua msanii anapotetereka anamuangusha shabiki wake anapotaka kujigamba kwa wenzake jinsi anavyomkubali msanii huyo.