Mwanamuziki maarufu wa nchini Kenya Anto Neosoul anajiandaa na ziara yake ya muziki Afrika Mashariki akianzia kwanza mjini Mombasa nchini Kenya mnamo tarehe 5 mwezi huu atakapotumbuiza na mwanadada Jaya.
|
Mwanamuziki Anto NEosoul wa nchini Kenya |
Anto Neosoul anayefanya vyema na wimbo wake uitwao 'Pay My Dues' amesema kuwa baada ya onesho hilo anatarajia pia kutua jijini Dar es Salaam na kupata fursa ya kukutana na wasanii mbalimbali nchini.
Aidha Anto NeoSoul ameelezea kuwa ziara hiyo kubwa Afrika Mashariki itachukua muda wa miezi minne.