Nyota imeanza kung'ara kwa kundi la Urban Boys ambao hivi karibuni wasanii hao wamelamba dili la kurekodi na kundi nyota la muziki Mafikizolo kutoka nchini Afrika Kusini.
|
Urban Boys |
Dili hilo limetua punde tu walipotoa wimbo wao mpya uliobatizwa jina 'Tayali' wakimshirikisha nyota wa nchini Nigeria Iyanya ukiwa ni wimbo unaofanya vyema katika stesheni mbalimbali nchini humo.
|
Mafikizolo |
Memba wa kundi hilo la Urban Boys Said Safi, amesema kuwa hivi sasa wanakamilisha nyaraka zote muhimu kwa ajili ya msafara wa kuelekea nchini Afrika Kusini kurekodi nyimbo na kundi hilo maarufu la Mafikizolo.