|
Mwanamke huyo baada ya kujifungua akiwa amezungukwa na watu waliokuwa wanamhudumia. |
MWANAMKE mmoja ambaye jina lake halikuweza kujulikana mara moja, aliwashangaza wapita njia katika jiji la Birmingham, Uingereza, majuzi baada ya kujifungua mtaani nje ya dula na nguo la Primark. Mama huyo alijifungua salama-salmin mtoto wa kike baada ya kuzidiwa uchungu akiwa kando ya barabara.
|
Watu wa huduma za afya wakiwa wamemzungushia mashuka ‘mzazi’ huyo. |
Wapita njia waliokuwa wakipita mtaani majira ya saa nane alasiri walimtafutia gari la wagonjwa, wakamwekea mablanketi chini na kumzungushia mashuka mama huyo ambaye alikuwa amelala chini ili kumsitiri.
|
Magari ya huduma yakiwa yamefika kumchukua mama na mwanawe katika duka la Primark. |
Watu wengi walifikiri kulikuwa na onyesho fulani mtaani hapo, lakini wakagundua ni mama huyo alikuwa amejifungua. Mama na mtoto walipelekwa Birmingham City Hospital kwa huduma zaidi.