Mahost wa Show ya Tanzania Movie Talents (TMT) Joti na Lulu wakiwa kwa Steji tayari kwa Show kuanza. |
Katika Onyesho hili litakalorushwa katika Runinga ya ITV siku ya Jumamosi saa 4 usiku kitakuwa kipindi cha kwanza kwa watanzania kuanza kuangalia na kuwapigia kura washiriki ambao watakuwa wamewavutia na kukonga nyoyo zao na hatimaye kuwawezesha kushiriki katika fainali kubwa Mwishoni mwa Mwezi wa Nane.
Watanzania wanatakiwa kuendelea kutazama muendelezo wa vipindi vya TMT kupitia Kituo cha Runinga cha ITV saa nne Usiku siku ya Jumamosi na hatimaye kuanza kuwapigia kura washiriki. Ili kuweza kupata Taarifa za TMT unaweza kutuma neno "TMT" kwenda namba 15678
Mchujo kwa washiriki sasa waanza rasmi ili kuweza kumpigia kura mshiriki umpendae unatakiwa kutuma neno "TMT ikifuatiwa na namba ya Mshiriki" kwenda namba 15678