Baadhi ya wachezaji wa Timu za Mkoa wa Dar es salaam wakichuana katika moja ya mchezo wa Ligi ya Mkoa Msimu Uliopita |
Kaimu Mkurugenzi mtendaji wa RBA Jimmy Nkongo amesema kwa kawaida wanatarajia kuwa na timu 16 lakini kabla ya kushiriki zinatakiwa kukamilisha malipo ya timu zao yakiwemo ada za Mwaka, Ada za Usajili na Ada za Ushiriki.
Nkongo amesema hadi kufikia muda huo uliopangwa kama kuna timu itakuwa haijakamilisha malipo hayo kwa mujibu wa sheria za Chama timu hiyo itakuwa imejitoa katika ushiriki wa michuano hiyo kwa mwaka huu.