Mtayarishaji wa muziki Tanzania Tudd Thomas ndiye aliyetayarisha wimbo wa Diamond ‘MdogoMdogo’ ambao unafanya vizuri sana pamoja na wimbo wa Ommy Dimpoz ‘Ndagushima’ ambazo zote zimepata nafasi kubwa huku wasanii hao wakilipa mamilioni kufanya videos.
Akiongea katika kipindi cha Sunrise cha 100.5 Times Fm na Fadhili Haule, Tudd amesema kuwa alilipwa kiasi cha shilingi milioni mbili kwa kila wimbo katika nyakati tofauti.
“Kikawaida huwa wanasema sio vizuri kwa kuwa ni biashara lakini mimi niko real, ni two million kwa kila wimbo.” Alisema.
Ameeleza kuwa gharama za nyimbo hizo zilitokana na ukubwa wa nyimbo zenyewe na muda alioutumia kukaa studio na wasanii hao.
Tudd amesema wimbo wa ‘MdogoMdogo’ ulitengenezwa kwa muda wa miezi mitatu kwa kuwa ulikuwa wimbo mgumu kwao wote kwa kuwa ilikuwa idea mpya kwa wote, wakati wimbo wa Ommy Dimpoz ulimchukua miezi miwili kuukamilisha.
Credit TimesFm
Friday, July 18, 2014
Tudd Thomas ataja kiasi alicholipwa na Diamond na Ommy Dimpoz kufanya 'MdogoMdogo na Ndigushima'
Labels:
Entertainment