Select Menu

Ads

Random Posts

Powered by Blogger.

Design

Technology

Circle Gallery

Shooting

Racing

News

Bottom

Thursday, July 3, 2014

Video: Obama Akiongea Na Tim Howard kwa njia ya Simu

Rais wa Marekani Barack Hussein Obama, ameendelea kuonyesha mapenzi na kikosi cha timu ya taifa ya nchi hiyo, ambacho siku mbili zilizopita kilishindwa kufanikisha safari ya kutinga kwenye hatua ya robo fainali ya michuano ya kombe la dunia huko nchini Brazil.

Obama, ameonyesha kuwa pamoja na wachezaji wa The Yanks, baada ya kupiga simu kwenye kambi ya timu ya taifa ya Marekani na kuzungumza na nahodha Clint Dempsey pamoja na Tim Howard, ambapo amesikika akiwapopngeza kwa niaba ya wachezaji wenzao.

Obama, hakusita kumpa shukurani mlinda mlango Tim Haward kwa kazi nzuri aliyoifanya wakati wote wa michuano ya kombe la dunia ambapo alionekana kuwa kisiki kwa timu pinzani pale walipolishambulia lango la USA.

Hata hivyo raisi huyo wa Marekani amemtaka mlinda mlango huyo wa klabu ya Everton ya nchini Uingereza, kujitayarisha na mapokezi makubwa kutoka kwa mashabiki wa soka nchini humo, kufuatai kazio nzuri aliyoifanya.
Katika kufikisha salamu hizo Obama amemkebehi Howard, kwa kumwambia kutokana na maandalizi yanayofanywa na mashabiki huko nchini Marekani, hana budi kukata ndevu ili kupunguza usumbufu, ambao utapoteza kumbu kumbu kwa walio wengi kuitokana na shauku waliyonayo dhidi yake.

Katika hatua nyingine Obama amewaambia wachezaji wa timu ya taifa ya Marekani ni vipi alivyoumizwa na hatua ya kutolewa kwenye fainali za kombe la dunia za mwaka huu, lakini akawasisitiza kutokuwa na hofu yoyote kwani mpango mkakati wa nchi hiyo kwa sasa ni kutaka kuona soka linachezwa kuanzia ngazi ya vijana wenye umri mdogo