Mwimbaji Christina Aguilera meamua kupiga picha akiwa mtupu kwa ajili ya jarida la ‘V Magazine’ la mwezi huu.
Katika picha hizo, mwimbaji huyo mwenye umri wa miaka 33 na mjamzito anaekaribia kujifungua, ameonesha umbo lake akiwa na mwanae tumboni huku akiwa amejifunika sehemu ya kifua chake na mikono.
Inaelezwa kuwa Christina ndiye aliyemuita mpiga picha Brian Bowen Smith kwa lengo la kumpiga picha ili apate kumbukumbu pia kabla ya kujifungua.
Mwimbaji huyo ambaye ni jaji wa shindano la The Voice, tayari ni mama wa mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka sita aliyempata na mumewe wa zamani Jordan Bratman na sasa anatarajia kumpata mtoto wa pili na Matt.
Monday, August 4, 2014
Picha: Christina Aguilera apiga picha akiwa mtupu kuonesha ujauzito wake
Labels:
Entertainment,
Life Style,
Photos