Kampuni ya Lionsgate imeamua kuchukua hatua ya kisheria dhidi ya tovuti za Torrent kwa madai ya kuvujisha filamu ya The Expandables 3 wiki mbili kabla ya kuachiwa rasmi.
Lionsgate imezitaja tovuti hizo kuwa ni Limetorrents.com, Billonuploads.com, Hulkfile.eu, Played.to, Swantshare.com, na Dotsemper.com.
Katika kesi hiyo, kampuni hiyo kubwa ya filamu inadai kuwa ilituma barua nyingi kwa kila tovuti ikiwataka kuiondoa Expandables 3 tangu July 26 hadi July 31 lakini tovuti hizo hazikujibu chochote.
Lionsgate wanataka mahakama itoe amri ya kusitisha kuendelea kuitumia filamu hiyo na pia kulipia fidia kwa hasara walioisababishia kampuni hiyo.
The Expandables 3 imeshakuwa downloaded kwenye mitandao zaidi ya mara milioni moja, lakini inatakiwa kuoneshwa kwa mara ya kwanza katika majumba ya cinema ya Marekani kuanzia Agust 15 mwaka huu.
Filamu hiyo imeandikwa na Sylvester Stallone aka Rambo, na kuwakutanisha waigizaji wakubwa kama Jet Li, Harrison Ford, Mel Gibson, Wesley Snipes, Victor Ortiz, Dolph Lundgren na wengine.
Monday, August 4, 2014
Kampuni ya Lionsgate kuzishitaki tovuti za Torrent kwa kuvujisha 'The Expandables 3'
Labels:
Entertainment,
Movie