Select Menu

Ads

Random Posts

Powered by Blogger.

Design

Technology

Circle Gallery

Shooting

Racing

News

Bottom

Monday, August 4, 2014

Diamond & Ali Kiba: G- Lover aelezea tofauti yao, asema Diamond aliisifia sauti ya Ali Kiba

Diamond Vs Ali Kiba ni ushindani usio rasmi unaochochewa zaidi na mashabiki wa muziki Tanzania kwa kuwa wawili hao licha ya kuwa wote ni wasanii wenye uwezo mkubwa sana kwenye uimbaji wanatajwa kuwa na tofauti au vita baridi. 
Wapo wengi ambao wanauzungumzia hata kama sio kwenye vyombo vya habari na kuna wachache ambao maoni yao yamefika kwenye vyombo vya habari. 

Vijimambo imezungumza na mmiliki wa G Records, Guru Ramadhani aka DJ G-Lover ambaye studio yake ndiyo ilimtoa Ally Kiba na kumfikisha kwenye mkondo mkubwa wa muziki ametoa maoni yake kuhusu utofauti anaouona kati ya wasanii hao.  Guru anaamini kuwa Ali Kiba ana hazina kubwa ya sauti na anakumbuka kuwa Diamond aliwahi kuisifia. 

Kwa kweli tofauti ukija kwenye masuala uimbaji, wengi wanaongelea hata katika mitandao tofauti tofauti kwamba Ali ana sauti nzuri na anaimba vizuri. Hata Diamond kuna wakati alikuwa anakiri kwamba angekuwa ana sauti kama ya Alikiba basi angefanya mambo makubwa zaidi.” Amesema G-Lover.  
Kwa mujibu wa G-Lover, wakati Ally Kiba yuko juu kupitia studio yake alikuwa na team ya watu wasiopungua thelathini, kitu ambacho Diamond anakifanya sasa hivi. 

Lakini unapokuja kibiashara Diamond huwa anazungumza kuwa yeye muziki wake anaufanya kibiashara na ndo maana ana team work kubwa ambayo inamsaidia yeye kujua ni kitu gani anatakiwa kufanya, kuna kitu gani anatakiwa kukifanya kwa upande wa muziki. Sasa kwa upande wa Ali kwa sasa hivi, kwa kipindi niko naye nilikuwa na team ambayo hata yeye alikuwa hajui mimi nipo na akina nani nyuma yangu. Alikuwa anajua kuwa yupo G, lakini nyuma yangu nilikuwa na watu takriban thelathini ambao ni team work ambayo ilikuwa inafanya kazi kwa Ali Kiba kujua ni kitu gani na kitu gani tunatakiwa tufanye ili afike na mpaka akafika hapo. Ameeleza.

Diamond naye anafanya vitu kama hivyo, unaweza kuona Diamond ana team ya watu watatu tu au wanne ambao wanamsaidia, kwahiyo utaona Diamond kuna watu kibao ambao amewapa ajira. Kwahiyo Diamond hawezi kuwaangusha watu ambao wapo nyuma yake ambao wamepata ajira kutoka kwake. Kwa mfano kuna utofauti mkubwa ambao Diamond amekuja nao ambao ukiangalia ni utaratibu uleule ambao nilikuwa nikiufanya kwa Ali. Kwahiyo sijui kuna utofauti gani kati ya management ya Diamond na ya Ally Kiba ya sasa hivi.” 
Credit: Vijimambo