Select Menu

Ads

Random Posts

Powered by Blogger.

Design

Technology

Circle Gallery

Shooting

Racing

News

Bottom

Thursday, July 24, 2014

Jokate asaka mwanaume wa kumuoa, ataja vigezo pia

Katika kuonyesha amechoshwa na upweke, mwanamitindo Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ ameibuka na kusema kuwa sasa anasaka mwanaume wa kumuoa huku akitaja vigezo vya anayestahili kumuita mume.

Akizungumzia maisha yake ya kimapenzi, Jokate alisema kuwa hana ‘mtu’ ila atakapotokea mwenye vigezo anavyotaka, hatakuwa na sababu ya kumkataa. “Kwa sasa sina mpenzi wala mchumba, akitokea sina kipingamizi ila mbali na vigezo vingine awe na mapenzi ya dhati na mimi,” alisema Jokate. 

Jokate amekuwa msiri sana katika maisha yake ya kimapenzi kiasi cha wengi kuamini ni msichana anayejiheshimu sana ila aliwahi kuwa na uhusiano na mchezaji wa mpira wa kikapu, Hasheem Thabeet anayekipiga kwenye Timu ya Oklahoma City Thunder ya nchini Marekani.