Watengenezaji wa bia na vinywaji vikali, wametishia kufunga baadhi ya viwanda iwapo Serikali haitaipunguza ongezeko la kodi la asilimia 20 iliyolipishwa kinyume na tozo ya asilimia 10 iliyopitishwa na Bunge.
Uamuzi huo umekuja baada ya wenye viwanda vya vinywaji hivyo kubaini kuwa Muswada wa Sheria ya Fedha wa mwaka 2014/15 uliotolewa Julai 11, mwaka huu, unataja kuwa kodi kwa bidhaa hizo itakuwa asilimia 20.
Akizungumza jana, mwakilishi wa wenye viwanda nchini, David Mgwassa alisema uamuzi wa kupandisha kodi kinyemela umewaacha njiapanda wenye viwanda kwa kuwa hawajui walipe kodi ipi kati ya asilimia 10 au 20 na kwamba, iwapo Serikali haitapunguza, watafunga baadhi ya viwanda ili kumudu ongezeko hilo jipya la kodi.
“Kila kampuni inafanya utafiti ili kufunga viwanda vyote na kubaki na kimoja kikubwa kitakachopunguza gharama. Pia ikumbukwe kuwa kuna viwanda vilijengwa kwa lengo la kuja kubinafsishwa, hivyo wengi watakosa ajira. Wawekezaji wana wasiwasi kama Tanzania ni sehemu nzuri kuwekeza tena.
“Kodi ya mwaka 2014 ni ipi? Viwanda vilipanga bei kulingana na asilimia 10, lakini Muswada wa Sheria ya Fedha unasema kodi hiyo imeanza rasmi kutoka Julai 1, mwaka huu, tutafilisi viwanda,” alisema Mgwassa.
Pia alihoji: “Kwa nini Bunge lijadili na kupitisha kodi asilimia 10 halafu muswada useme asilimia 20. Ni nani anayemtania mwenzake?”
Alisema iwapo mahitaji ya bidhaa hizo yatapungua nchini, kampuni zinazomiliki viwanda vya vinywaji zitalazimika kupunguza uzalishaji.
Alisema viwanda vya bia na vinywaji vikali vinapambana na ushindani mkali kutoka bidhaa za nje zinazoingia nchini kinyume cha sheria, jambo linaloweza kuufanya uchumi ukashuka iwapo hali hiyo haitadhibitiwa.
Credit Mwananchi.
Popular Posts
-
New Music: Chidi Benz Feat Bob Junior - Mahaba Niuwe
-
Download wimbo Kamili HAPA MKITO wa Msanii mdogo wa Umri Mkubwa wa akili aka "Jose G" akiwa amemshirikisha Legendary SpacDaw...
-
Baadhi wanawake siku hizi wamekuwa wakijiuliza vazi gan ambalo linafaa kuvaliwa wakati wa usiku na likawapendeza sasa unaweza kutazama pic...
-
KAULI ya nyota wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ kwamba hawezi kuoa kamwe, inadaiwa kumchefua mwandani wake, Wema Isaac Sepe...
-
Baadhi ya Mastar wa Tanzania wameamua kuweka wazi nia zao za kugombea nafasi za uongozi katika ngazi mbalimbali,miongoni mwa watu hao kwa ...
-
Wakati Michael Jackson akiwa amelala kwenye nyumba yake ya milele, bado familia yake imeendelea kuandamwa na tuhuma nzito zinazomhusu mfalme...
-
Siku 74 baada ya kufunga ndoa na Kanye West huko Florence, Italia Kim Kardashian amefuata taratibu za kisheria na kubadili jina lake rasmi k...
-
Kindumbwe ndumbwe cha michuano ya klabu Bingwa Afrika mashariki na kati maafuru Kagame Cup kinaanza kesho ambapo mechi ya ufunguzi ya Kund...
Advertisement
Advertisement
Advertisement With Us