Select Menu

Ads

Random Posts

Powered by Blogger.

Design

Technology

Circle Gallery

Shooting

Racing

News

Bottom

Sunday, July 6, 2014

Maua Sama amtaja Mwana FA kuwa mkombozi wake kimuziki

Nominee wa tuzo za KTMA 2014, Maua Sama, amesema ni Hamis Mwinjuma aka Mwana FA ndiye anayemchukulia kama mkombozi wake kwakuwa alimsaidia kurejesha tena ndoto zake za kimuziki kipindi alipokuwa amekata tamaa.   

Hitmaker huyo wa ‘So Crazy’, amesema alifahamiana na Mwana FA kupitia dada yake na rafiki yake ambaye alimtumia baadhi ya nyimbo za Maua alizokuwa amezirekodi mjini Moshi na sauti yake kumshawishi rapper huyo wa ‘Mfalme’. “Mwana FA alinisikia na hakutaka kipaji changu mimi kiishie hapo hapo,” Maua ameiambia Kikwetu Blog. “Kwasababu by the time ananigundua nilikuwa nimeshakata tamaa ya kuimba. Hakunifia tu, alininyanyua pia.” 

Amesema kilichokuwa kimemkatisha tamaa na kurekodi nyimbo kadhaa katika studio ndogo za Moshi ambazo hazikufika popote licha ya yeye kutumia gharama kuzikamilisha. Kingine Maua ambaye hivi karibuni aliachia wimbo wake mpya ‘Let Them Know’ wenye mahadhi ya reggae, amesema wakati huo pia mama yake alikuwa hataki afanye muziki na hivyo aliamua kujikita zaidi katika elimu.