Select Menu

Ads

Random Posts

Powered by Blogger.

Design

Technology

Circle Gallery

Shooting

Racing

News

Bottom

Sunday, July 6, 2014

Shaa apata shavu la kuwa jaji wa shindano la Sakata Mashariki

Muimbaji wa zamani wa kundi la Wakilisha na hitmaker wa Sugua Gaga, Sarah Kaisi aka Shaa amepata shavu la kuwa jaji wa shindano kusaka vipaji vya kucheza la Sakata Mashariki.

Shaa ameungana na jaji  kutoka Kenya aitwa Ian kwenye usaili wa Dar es Salaam uliofanyika Jumamosi hii.

Kwa mwaka huu Sakata Mashariki iliyoanzishwa na kituo cha runinga cha Citizen cha Kenya, inashirikisha nchi za Kenya, Uganda na Tanzania.

Haijafahamika kama Shaa ataendelea kuwa jaji katika mashindano hayo yatakayoendelea kufanyika jijini Nairobi pale vikundi mbalimbali kutoka nchini hizo tatu vikiaanza kushindana.