Select Menu

Ads

Random Posts

Powered by Blogger.

Design

Technology

Circle Gallery

Shooting

Racing

News

Bottom

Thursday, July 3, 2014

Mirror azungumzia muziki wake, kuwa chini ya kampuni ya Wema, Collabo na Chameleone, kusaka 'kick'

Mirror ni msanii anaefanya kazi chini ya kampuni ya Wema Sepetu, Endless Fame akiwa anasimamiwa kazi zake na Petit Man.

Msanii huyu ni moja kati wasanii waliofanya kazi kwa karibu na marehemu Ngwair na kuchangia kuzing’arisha nyimbo kama ‘Maskini Wenzangu’ na nyingine.

Kutokana na uwezo wake, Mirror alilikuna sikio la Jose Chameleone ambaye aliingia nae studio na kufanya wakapika wimbo mmoja ambao anauelezea kama kitu kingine kikubwa kutoka kwake.

Hivi sasa mwimbaji huyu anafanya vizuri na hits kadhaa kama Baby na KoloKolo.

Mirror amefanya mahojiano na Josefly Muhozi, mwandishi wa tovuti ya Times Fm na kufunguka mengi kuhusu maisha ya muziki wake, kuwa chini ya kampuni ya Endless Fame ya Wema Sepetu na kile anachotamani kisitokee kati yake n boss wake huyo, mpango wa kupelekwa shule ya muziki na kampuni hiyo na mengine ambayo hutakiwi kuyakosa.

Sikiliza hapa.

Credit TimesFM.